Ni siku ya inne katika msururu wa kugawa pesa ya kuanzisha biashar kwa vijana wa kenya ndani ya mradi wa kuinua vijana wa NYOTA. Kikundi kizima cha serakali kikiongozwa na Rais wa jamuhuri Mheshimwa Dkr William Ruto, leo kimetua Machakos katika hafla inayoleta gatuzi tatu za mashariki kusini, zikiwemo Machakos, kitui, na Makueni kutimisha shughuli hii muhimu.
Katika kufukia lengo tekelezi la serikali la kuinua vijana, Katibu katika Idara ya Vijan na Uchumi Bunifu Bwana Fikirini Jacobs Kahindi, Pamoja na mwenzake wa Idara ya Bisahara ndogo na za Kati, Bi Susan Auma Ma’ngeni, wamejisatiti vilivyo kuhakikisha asdhma ya serikali ya kuumalisha maisha ya vijana na kuwavika uwezo wa kujiendelesha kiuchumi na katika maisha imeafikiwa.
kwenye hafla ya leo takribani shilingi milioni 147.5 zimetolewa kwa vijana wapatao 5,901 kutoka kaunti za Machakos, Kitui na Makueni. Fedha hizi zitasaidia vijana wafaidi kuwekeza kwa biashara ndogo ndogo na kuanza safari ya kujimundu na kuchangia katika Uchumi wa taifa.
