NYOTA MOMBASA – UKANDA WA PWANI

Katibu Mkuu wa Masuala ya Vijana na Uchumi bunifu , Fikirini Jacobs, alijiunga na Rais Dkt. William Samoei Ruto leo katika Uwanja wa Jomo Kenyatta, Mkomani, Mombasa, wakati wa zoezi la ugawaji wa ruzuku ya kibiashara ya NYOTA yenye thamani ya Shilingi milioni 147 kwa vijana 5,880 kutoka gatuzi la Mombasa, Taita Taveta na Kwale.

Katika hotuba yake, Katibu Jacobs alielezea mradi wa NYOTA kuwa ni jitihada muhimu ya Serikali inayolenga kuwawezesha vijana kiuchumi.

Alisisitiza kuwa ruzuku hio inatolewa kwa uwazi na bila mapendeleo ya kisiasa au kibinafsi, huku akiwahimiza wanufaika kutumia fedha hizo kwa uwajibikaji ili kukuza biashara zao.

Bw. Jacobs pia alibainisha kuwa mpango wa NYOTA hauishii katika utoaji wa fedha pekee, bali unawapa wanufaika fursa ya kupata ushauri, mafunzo na msaada endelevu ili kuhakikisha mafanikio ya muda mrefu ya biashara zao.